Thursday

JCB-Kuuza Album yake mkononi

JCB

Msanii wa kizazi kipya Jacob Makalla a.k.a JCB ambaye anatamba na track yake inayozidi kuwa juu kila siku zinavyozidi kwenda ya Ukisikia Paah remix ambayo amewashirikisha wasanii wa Hip Hop Fid Q, Jay Moe na Chidi Beenz amesema mashabiki wake wategemee makubwa na Mengi kutoka kwake.
Msanii huyo amejigamba kwa kuachia albam yenye jumla ya nyimbo 16 huku akielezea ukimya wake kuwa kujipanga upya na sasa amerudi madini ya ajabu. Kwa sasa nina mistari ya ajabu,wapinzani wake Mjifiche!’ Alisema msanii JCB.
 
JCB amezitaja baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni Movement of silence,Kijiti,Kijenge ya juu,Usinitafute,Prison break,Ninapo,arusha na nyinginezo,anasema na kuongeza kuwa albamu hiyo imerekodiwa ndani ya studio za Watengwa chini ya prodyuza David Bakari a.k.a Daz.
JCB anayetokea pande za Arusha hususan kundi la Watengwa, alisema kuhusu kundi hilo kwamba,wamepunguza speed kwani baadhi ya wasanii hao wako safarini Sweden akiwemo Chindo man.
Aliongezea kwamba hakuna kitu kilicho haribika kwani ni muda mfupi watakuwa wameshatimba Arusha na hapo ndipo wataanza kuachia vitu vile vilivyo sababishsha tukawa kimya.
JCB amebainisha kuwa albamu hiyo iliyojaa kila aina ya maudhui inauzwa buku kumi tu.Ukiitaka basi wasiliana nae kwa namba yake ya kiganjani
0713641677
0784641677

No comments:

Post a Comment